Hello;
Habari yako ndugu yangu karibu katika somo hili jipya la mafunzo ya ufundi simu kwani nimekuletea somo la mafunzo ya ufundi simu kwa kutumia kompyuta ungana nami hatua moja kabla ya nyingine ninatumaini hatimaye utatoka na kitu fulani.Mafunzo yetu yamekita upande wa program yaani kwa kutumia kompyuta labda kwanza tujue je ufundi kwa njia ya programu (software) ni nini?
Nini maana ya ufundi simu
Ufundi simu ni marekebisho ya simu ya rununu(mkononi) au hata zile nyinginezo kama tablet na nyinginezo ufundi huu umekita katika pande kuu mbili ambazo ni upande wa programu(software) upande wa hardware yaani matengenezo yasiyo hitaji kompyuta lakini mafunzo yetu yamekita zaidi upande wa software
Je software ni nini?
Software ni matengezo ya simu ambayo hujihusisha zaidi na upande wa programu au mfumo matatizo haya hugawanyika katika sehemu nyingi na wakati mwaingine husababisha simu kutowaka kabisa(dead boot),kuwaka na kuishia njiani(boot loop),password protection,kufungiwa mtandao(sim lock),kutokuwa na uwezo wa kupiga simu na mengine mengi
Je utajuaje kama simu yako ina matatizo ya software?
Mara nyingi kabla ya kufanya marekebisho ya simu yako ni muhimu sana kuzingatia chanzo cha tatizo na mara nyingi kama tatizo limetokana na mfumo wa progamu wa simu basi hata utatuzi wake pia unatakiwa utatuliwe kwa programu.
Lakini vilevile kwa baadhi ya matatizo ya hardware hutegemea mfumo wa programu ili kukiwezesha kifaa chako kufanya kazi kwa mfano;pale simu inapobadilishwa baadhi ya vifaa kama chip mbalimbali,lcd display,touch screen na mengineyo ili kufananisha hardware id na software id.Ili kuweza kufahamu zaidi ni lazima ujue kuwa kuna aina ngapi za simu
Je kuna aina ngapi za simu?
kwanza ni vema tujue ya kuwa ili tuweze kutengeneza simu yetu kwa njia ya kompyuta ni lazima tuweze kuitofautisha kwa kulingana na kundi la simu,
kiufundi simu hutambulika kwa aina ya cpu yake hizi hugawanyika kwenye makundi tofauti na yafuatayo ni makundi yake
Mediatek

Hii ni chip inayotumika zaidi na makampuni mengi kutengeneza simu hasa asilimia kubwa ya simu za kichina kama vile Tecno,lenovo,infinix na mengineyo mengi
vifuatavyo ni vifaa(flashing tools) vinavyotumika kutengenezea zaidi

0 Comments